





































VIGOGOÕ wa MAISHA wanapokutana: Mhariri muasisi wa gazeti hili, Daniel Mwaijega (kushoto) akisalimiana na Hassan Abbas (katikati) na Amandus Mtani (kulia). Mwaijega kwa sasa ni miongoni mwa Wahariri wa gazeti la Mwananchi, Abbas alikuwa mwandishi mwandamizi wa gazeti hili (sasa ni Mhariri wa Habari wa Majira) na Mtani ni Mhariri wa sasa wa Maisha. ÔVingungeÕ hawa walikutana Ijumaa, Oktoba 17, 2008 kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni ya Business Times Limited wachapishaji wa magazeti ya Majira, Business Times, Spoti, Dar Leo na Maisha.
Mameneja mikoani ('wakuu' wa mikoa) wa Kampuni ya Business Times Limited wakiwa katika kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni hiyo wachapishaji wa magazeti ya Majira,Business Times, Spoti, Maisha na Dar Leo. Kutoka kushoto ni Hamza Gwandi-Iringa, Aziz Msuya- Morogoro na Crescencia Kapinga-Ruvuma.

























