Wednesday, July 9, 2008

Sherehe ya kumuaga aliyekuwa Meneja Mkuu wa Business Printer Ltd Mrs. Getrude Nyaulawa

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Business Printers Ltd (BPL), Bw. Rashid Mbuguni (kushoto) akimkabidhi aliyekuwa Meneja Mkuu wa BPL, Bibi Getrude Nyaulawa, cheti cha utumishi uliotukuka, baada ya kuitumikia kampuni kwa miaka 18. Bibi Nyaulawa aliyestaafu kazi kuanzia Juni mwaka huu, aliagwa rasmi na kampuni za BPL, Business Times Ltd na Radio Times katika viwanja vya ofisi hizo, mtaa wa Lugoda, Dar es Salaam.Aliyekuwa Meneja Mkuu wa BPL, Bibi Getrude Nyaulawa, akitoa hotuba fupi kwa wafanyakazi waliohudhuria tafrija hiyo ya kuagana naye mara baada ya kustaafu Kaimu Meneja Mkuu wa BTL, Bw. Aga Mbuguni akizungumza wakati wa tafrija hiyo.Mkurugenzi Mtendaji wa BPL, Bw. Rashid Mbuguni akizungumza wakati wa hafla hiyo.Kaisi John akiimba shairi alilotunga rasmi la kumuga Bi. Getrude Nyaulawa wakati wa tafrija hiyo.Mkurugenzi Mtendaji wa Business Printers Ltd (BPL), Bw. Rashid Mbuguni (kushoto) akijadiliana jambo na aliyekuwa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Bi. Getrude Nyaulawa (katikati) na Naibu Meneja Mkuu wa BPL, Bw. Samson Ndalichako wakati wa sherehe ya kumuaga Bi. Nyaulawa aliyestaafu kazi. Sherehe hizo zilifanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo, Lugoda, Dar es Salaam.Mwanasheria wa kampuni za BPL, BTL na Radio Times FM, Bw. Mabere Marando (kushoto) akigongeana bilauri na Meneja Mkuu anayestaafu wa BPL, Bi Getrude Nyaulawa wakati wa tafrija ya kumuaga. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa BPL, Bw. Rashid Mbuguni
Mhairi Mkuu wa gazeti la Majira, Bw. Joseph Kulangwa akigongena glasi na Meneja Mkuu anayestaafu wa BPL, Bi. Getride Nyaulawa (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa BPL, Bw. Rashid Mbuguni wakati wa tafrija ya kumuaga Bi. Nyaulawa.Mkurugenzi wa Radio Times FM, Bw. Rehure Nyaulawa (kulia) akigonganisha glasi na Mama yake mzazi, Bi. Getrude Nyaulawa (kushoto) aliyekuwa Meneja Mkuu wa BPL ambaye sasa anastaafu kazi wakati wa tafrija ya kumuaga.
Wafanyakazi wa makampuni ya BPL, BTL na Radio Times FM wakiserebuka. dah!!
Mambo yalivyokuwa wakati wa tafrija ya kumuaga Bi. Getrude Nyaulawa. Dah!! hapo hatuna cha kuongeza watu wangu ni fully kujiachiaBi. Getrude Nyaulawa akisalimiana na Mkaguzi wa Ndani Mwandamizi Msaidizi wa BTL, Bw. Charles Sichalwe, mwenye tisheti nyeusi ni ICT Officer wa kampuni ya BTL ndugu Kenneth Nchimbi, huku anayetabasamu kulia ni mhariri mkuu wa gazeti la Maisha ndugu Mtani pamoja na wafanyakazi wengine wakati wa tafrija ya kumuaga.

Ni wakati wa chakula hapo... Kushoto ni Meneja Usambazaji wa BTL, Bw. Samwel Petro na Bw. Charles Sichalwe, Mkaguzi wa Ndani Msaidizi Mwandamizi wa BTL.Bi. Getrude Nyaulawa akipokea zawadi kutoka kwa wafanyakazi wenziwe wakati wa tafrija hiyo. Anaye kabidhi zawadi mbele ni Christina Ntole huku baadhi ya wadau wakifuata nyuma kwa mbwembwe zote

Kinamama wa makampuni ya BPL, BTL na Radio Times FM wakimvisha kitenge Meneja Mkuu anayestaafu wa BPL, Bi; Getrude Nyaulawa wakati wa tafrija ya kumuaga usiku huo


No comments: