Wadau kwa mechi tu hawajambo, Watu ndani ya uwanja wa taifa hawana noma huku wakisubiri kutizama mtanange wa kukata na shoka siku Cameroon ilipo shindwa kufua dafu ndani ya vijana wa Maximo.. Ila mapozi haya ni balaa..
Mdau wetu mmoja akiwa katika purukushani za hapa na pale kutimiza wajibu wake wa kila siku, alipo naswa na mpiga picha wetu katika kazi zake za kila siku. . dah!!!!!
Mdau wa michezo wa times 100.5fm akiwa na shamra shamra za furaha huku akirusha kipindi chake hewani kwa mashabiki wake wa kipindi hicho kinacho vuma siku hata siku kwa wakazi wa Dar, Pwani na huko Zenji... niliamua kuwa na mahojiano kidogo na mtu wangu Gwamaka: Mahojiano yangu nae yalikuwa kama hivi..wilmushi: Gwamaka mambo vip?
Gwamaka: Mzuka sana mtu wangu kwani vipi mbona umeniibukia huku kwenye kipindi mida hii?
wilmushi: Ebwana nimeona unavuma sana huko mitaani nikapenda kujua siri ya mafanikio yako Mwana..
Gwamaka: Wee kaa hapo uone siri ya mafanikio mtu wangu Mushi, ni kukamua kwenda mbele hakuna mchezo na fani za watu.
Bila kusita niliamua kukaa na kaangalia pindi linavyo ungurumishwa mida hiyo ya saa moja hadi moja na nusu...
wilmushi: Ebwana hapo sina ubishi mtu wangu naona makamuzi kwenda mbele kaka..
Gwamaka: Unalingine kaka?
Willy: Nina swali la kizushi tu... Hiyo Tishert imekutoa kinoma mtu wangu, niagizie basi na mie nikanunue..
Gwamaka: Dah!!! hahahhhahahaahahaaa.... acha kunienjoy Mushi, ni mambo ya sport haya. . . Hii ni Copa.
wilmushi: Za misaada huwa zinakutoa kichizi kaka
Gwamaka: Wee sema kama umezimia nikuuzie acha uzushi studio...
wilmushi: Ila unawapagawisha kichizi wasikilizaji wako, naona kipindi kinawashika kichizi mtaani huko... ok tutimke zetu kaka
Thanx Gwamaka
No comments:
Post a Comment